Jinsi ya kupika Chapati za maji: Leo
ninakuletea hatua kwa hatua namna ya kuandaa na kupika Chapati laini za Mayai.
Tafadhali fuatana nami katika pishi hili.
Pishi:
Chapati za maji/laini
Utangulizi: chapati ni kitafunwa au chakula kinachopendwa na wengi.
Kuna Chapati za Kusukuma na Laini au za maji. Aina hii ya pili hupendwa zaidi
na watu kwa sababu ni rahisi kutayarisha. Fuatana nami hatua kwa hatua namna ya
kuandaa pishi hili tamu
Mahitaji
- Ngano 1/2 kilo
- mayai 3
- mafuta au samli 1/4 kikombe
- kitunguu kikubwa kilichosagwa 1
- Kitunguu Swaumu punje 4
- Chumvi 1/2kijiko au kulingana na matakwa yako
Mahitaji
Namna
ya kupika chapati za maji
- Chekecha unga wako vizuri weka katika bakuli safi.
- Tia maji katika bakuli la unga na ukoroge mpaka upate uji wa wastani si mzito san a wala si mwepesi sana.
- Ongeza mayai na chunmvi endelea kukoroga.
- Ongeza kitunguu swaumu na kitunguu maji. Injika kikaango chako jikoni subiri kipate moto.
- Chota pawa moja mimina na tandaza kuzunguka kikaango subiri sekunde tano hadi kumi mpaka ikauke kisha geuza upande wa pili.
- Tia mafuta huku ukigeuza na kuzungusha ili mafuta yaenee pande zote na ili chapati isiungue. Endelea kugeuza mpaka iwe rangi ya kahawia.
- Hapo chapati zitakua tayari kwa kuliwa.
- Fanya hivyo kwa chapati zote zilizobakia
Matayarisho hayo yanatosha kupika
chapati za mayai/laini sita (6) mpaka kumi (10) . Chapati za maji hupendeza
zaidi kuliwa Michuzi mizito, Chai na kadhalika. Nenda kajaribu kuandaa pishi
hili kisha uje utupe mrejesho. Kama una maoni yoyote kuhusu Jinsi ya kupika
chapati za Maji na Mayai andika hapo chini. Asante
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni