Jumatatu, 23 Oktoba 2017

JINSI YA KUPIKA WALI NA NGEGERE



Tangu nilipokuwa mdogo ilikuwa siku wakipika njegere na tukala na wali kusema kweli nilikuwa nafurahi kiwango kikubwa sana. Zaidi pale inapokuwa njegere zimeungwa na tuzi zito la nazi. Sasa nishakuwa mtu mzima na najua kupika hivyo mara nyingi huwa najipikia.
Hili ni pishi moja rahisi sana kwa yeyote anaweza pika bila kukosea. Mahitaji ya kawaida tu ni njegere, nazi, vitunguu , nyaya ila sasa kuna ziada ili kuongeza nakshi nakshi na ndio mimi sasa leo nakuelekeza vile ambavyo mimi huwa napika
MAHITAJI
  • Glass 3 za njegere
  • Vitunguu maji viwili – vikatwekatwe
  • Nyanya 3 – Zimenywe na kukatwa katwa
  • Karoti moja – Ikatwe vipande vidogo dogo
  • Mchanganyiko wa Kitunguu swaumu na Tangawizi kijiko 1 cha chai
  • Mahanjumati masala kijiko 1 cha chai – Waweza tumia spice mix aina yoyote ikiwa hauna Mahanjumati masala
  • Tui zito la nazi Glass moja 1
  • Mafuta ya kula vijiko 3 vya mezani
JINSI YA KUPIKA
  1. Kwanza chemsha njegere zako hadi kuiva ila sio kurojeka – zikiwa tayari weka kando
  2. Weka chombo unachotumia kuunga mboga na uweke mafuta yakiaanza kupata moto weka vitunguu maji na endelea kukaanga hadi vilainike
  3. Vikiisha kulainika weka ule mchanganyiko wa kitunguu swaumu na tangawizi. Endelea kuvipika vikiwa kama vinaanza kubadiri rangi sasa weka zile nyanya.
  4. Zipike nyanya hadi zitakapoiva na kuwa kama zinatengana na mafuta ndipo unaweka karoti na mahanjumati masala au spice mix ulionayo kwa sekunde chache kisha unaweka njegere
  5. Ili zisiwe kavu sana unaweza ongeza kidogo yale maji yaliyotumika kuchemsha njegere. Ongeza na chumvi kiasi upendacho. Kisha mchanganyiko huo uendelee kuchemka kwa dakika 3-4
  6. Sasa weka lile tui la nazi na punguza moto. Baada ya kuweka tui la nazi endelea kukoroga kwa dakika chache hadi itakapoanza kuchemka taratibu. Baada ya hapo epua na tayari kwa kula.
Furahia pishi hili zuri la Njegere Nazi. Hapa chini nimeweka video nikionyesha jinsi ya kukuna nazi na kutengeneza tui la nazi.





Hakuna maoni:

Chapisha Maoni